Onana: Tutatoa Kila Kitu Leo

Golikipa wa Manchester United na timu ya taifa ya Cameroon Andre Onana amezungumza na waandishi wa habari na kusema usiku wa leo watajitoa sana kuhakikisha wanapata alama tatu.

Onana amezungumza na waandishi wa habari na kusema hawezi kuwaahidi ushindi moja kwa moja ila ambacho anaweza kukisema ni kua watapambana na kutoa kila kitu uwanjani kuhakikisha wanapata alama tatu.OnanaManchester United leo watashuka dimbani wakiwa ugenini katika dimba la Allianz Arena dhidi ya klabu ya Fc Bayern Munich katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa ulaya.

Golikipa huyo alielendelea kwa kusema wanapaswa kuota kwa ukubwa na sio mdomoni tu bali wanapaswa kuonesha dimbani, Huku akikiri msimu umeanza tofauti na walitaka lakini anaamini utamalizika wakiwa bora zaidi ya walivyoanza.OnanaManchester United wanakwenda kumenyana na Bayern Munich wakiwa kwenye kiwango kibovu kwani wameanza vibaya ligi kuu ya Uingereza wakipokea vipigo vitano katika michezo mitatu, Lakini Onana anaamini leo wanapaswa kupambana na kuuanza msimu kwa namna nyingine kabisa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.