KOCHA MPYA SINGIDA ANG'ATUKA

INAELEZWA kuwa Kocha Mpya wa klabu ya Singida Fountain Gate raia wa Ujerumani Ernst Middendorp (64) jana Jumatatu aliandika barua ya kung’atuka kikosini humo huku sababu ikiwa ni kuingiliwa na viongozi klabuni hapo kwenye majukumu yake.

Mpaka muda huu Viongozi wa Juu wa klabu ya Singida Fountain Gate wanahaha kujua alipo wakati Simu zake zote zikiwa zimezimwa (hapatikani),singidaChanzo cha habari kimethibitisha kuwa, Kocha amechukizwa na Viongozi wake klabuni ya Singida Fountain Gate kutaka kumpangia wachezaji wa kucheza Kwenye mchezo wao dhidi ya Future.

Juhudi za Kutaka kujua alipo zinaendelea ili wazungumze nae na arejee kwenye majukumu yake klabuni hapo. Huku pia Meridian Sports ikiwa macho kufuatulia ukweli wa Taarifa hii.

Acha ujumbe