Bellingham Nje Mwezi

Kiungo wa klabu ya Real Madrid Jude Bellingham anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa takrribani mwezi mzima kutokana na majeraha ya msuli aliyoyapata.

Bellingham amepata majeraha hayo kwenye mazoezi ya timu hiyo na kocha Carlo Ancelotti amethibitisha mchezaji huyo amepata majeraha hayo, Huku taarifa ya klabu ikieleza kua mchezaji huyo atakaa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja na atakosa michezo kadhaa ya ligi hiyo.bellinghamBellingham atakosa michezo mitatu ambayo ni kati ya Real Valladolid, Real Betis, pamoja na Las Palmas akitarajiwa kurejea kati michezo miwili dhidi ya Real Sociedad, Espanyol mabingwa wa ulaya klabu ya Real Madrid itapaaswa kumchezesha mchezaji mwingine ili kuziba pengo la Muingereza huyo.

Wachezaji ambao wanatajwa wanatarajiwa kuvaa viatu vya Bellingham katika michezo ya ambayo kiungo huyo wa zamani wa Dortmund atakosekana ni Luca Modric, pamoja na kinda Arda Guler viungo hao ndio wanaonekana wataweza kutoa ambacho alikua anakitoa Jude ndani ya timu hiyo.

Acha ujumbe