Kiungo wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Ufaransa Eduardo Camavinga anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki zisizopungua saba baada ya kuumia siku ya jana katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Uefa Super Cup dhidi ya Atalanta.
Camavinga alipata majeraha katika goti lake la kushoto siku ya jana akiwa mazoezini na kushindwa kuendelea na mazoezi na wenzake, Klabu ya Real Madrid ilikua inasubiri uchunguzi wa madaktari juu ya ukubwa wa jeraha na taarifa zilizotoka kiungo huyo atakaa nje ya uwanja kwa wiki saba.Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua moja ya wachezaji muhimu kwa klabu ya Real Madrid tangu ajiunge klabuni hapo mwaka 2021, Lakini umuhimu wake umeongezeka zaidi kipindi hiki ambacho Toni Kroos amestaafu hivo ni wazi ni pigo kwa klabu hiyo kuelekea mwanzo wa msimu huu.
Taarifa zinaeleza kiungo Camavinga atarejea ndani ya timu hiyo mwenzi Oktoba jambo ambalo litawapa wakati mgumu kidogo klabu ya Real Madrid, Lakini timu hiyo ina machaguo mengine kwenye eneo la katikati kwa wachezaji kama Valverde, Ceballos, Modric, pamoja na Aurellien Tchoumeni.