Bruno Fernandes Asaini Kandarasi Mpya ndani ya Man United

Nahodha wa klabu ya Manchester United kiungo Bruno Fernandes kama ambavyo ilielezwa siku kadhaa zilizopita kua yupo mbioni kusaini mkataba mpya ndani ya timu hiyo na inaelezwa leo mchezaji huyo amemwaga wino wa kuendelea kuitumikia klabu ya Man United.

Bruno Fernandes mkataba wake haukua umemalizika ndani ya klabu hiyo na ulikua unamalizika mwaka 2026 lakini Man United wameamua kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine mmoja, Hivo mkataba aliousaini Bruno leo utamuweka klabuni hapo mwaka 2027.bruno fernandesKiungo huyo wa kimataifa wa Ureno ameonesha kiwango cha hali ya juu sana ndani ya Manchester United tangu ajiunge na timu hiyo mwezi Januari mwaka 2021, Hii imesababisha benchi la ufundi pamoja na mabosi wa klabu hiyo kuhitaji kuendelea kupata huduma ya kiungo hiyo kwa muda mrefu zaidi.

Kwa maana hiyo kiungo Bruno Fernandes ataendelea kuwepo ndani ya Manchester United kwa miaka mingine mitatu bila kusahau kipengele cha kuongeza mwaka mwingine mmoja ambao itakua mpaka 2028, Hivo kama kiungo huyo atakubali kukifata kipengele cha mwaka mmoja basi atasalia klabuni hapo kwa miaka minne badala ya mitatu.

Acha ujumbe