Kiungo wa zamani wa klabu ya Fc Barcelona Andres Iniesta ameonesha imani yake kwa kocha wa klabu hiyo Xavi Hernandez kiungo mwenzake wa zamani ndani ya klabu hiyo.

Fc Barcelona ambao wametolewa kwenye ligi ya mabingwa ulaya msimu huu ikiwa ni mara ya pili mfululizo, Klabu hiyo kushindwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo jambo ambalo linawafanya mashabiki wa klabu hiyo kumnyooshea kidole kocha wa klabu hiyo Xavi Hernandez.iniestaKiungo huyo wa zamani wa klabu hiyo yeye anaamini kocha Xavi atafanya vizuri ndani ya timu hiyo licha ya kunyooshewa vidole kutokana na mwenendo wa klabu hiyo siku za hivi karibuni chini ya mwalimu huyo.

 

Kiungo Iniesta yeye anaona licha ya changamoto ambazo anakutana nazo Xavi katika wakati huu lakini kocha huyo atafanya vizuri na timu hiyo siku za mbeleni kwasababu ni mtu anaeijua timu hiyo zaidi.iniestaKiungo huyo kwasasa anaitumikia klabu ya Vissel Kobe ya nchini Japan huku akikataa kuweka wazi juu ya suala la yeye kujiunga na mchezaji mwenzake huyo wa zamani kwenye ukocha.

Andres Iniesta na Xavi wanakumbukwa zaidi kwenye ulimwengu wa soka kwa kutengeneza utatu mtakatifu kwenye eneo la katikati ndani ya klabu ya Barcelona wakiwa wachezaji wakisaidiwa na Sergio Busquets.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa