Kiungo wa zamani wa klabu ya Real Madrid Isco Alarcon anaendelea kuwasha moto ndani ya klabu yake ya sasa ya Real Betis inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania.
Isco amekua na mwendelezo wa kiwango bora tangu ajiunge na Real Betis katika majira ya joto yaliyopita kwa uhamisho huru, Jambo lilimfanya kua moja ya wachezaji tegemezi ndani ya klabu hiyo.Kiungo huyo amefanikiwa kua nyota wa mchezo mara sita mpaka sasa katika michezo kumi ambayo ameitumikia klabu ya Real Betis katika ligi kuu ya Hispania msimu huu.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania mkataba wake unamalizika mwaka 2025 ndani ya timu hiyo, Lakini kuna kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja bila kusahau kipengele cha Euro milioni 10 kiasi kitakachoweza kumtoa klabuni hapo.Kiungo Isco Alarcon amewashangaza wengi kutokana na kiwango ambacho amekionesha ndani ya Real Betis, Kwani kiungo alikaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita bila kua na timu baada ya kuondoka Sevilla lakini amerudi uwanjani na kuonesha ubora mkubwa.