Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta ameweka wazi hawajawahi kufikiria kumfuta kazi kocha wao wa sasa Xavi Hernandez kwakua ni mtu anayeijua Barcelona na klabu hiyo itaimarika chini ya kocha huyo.

Rais huyo amezungumza hayo alipokua anafanya mahojiano na kituo kimoja cha habari nchini Hispania na kueleza wao kama uongozi wa klabu hiyo hawajawahi kufikiria kumfuta kazi Xavi kutokana na mwenendo wa klabu hiyo kwasasa.laportaKlabu ya Barcelona imekua na mwenendo ambao sio mzuri chini ya Xavi lakini Rais Laporta amesisitiza bado wapo na kocha huyo tena kwa asilimia mia moja ataendelea kubaki hapo na sababu kubwa ni kwakua Xavi ni mtu ambaye anaijua klabu hiyo na imani kubwa imewekwa kwake wakiamini ataiimarisha klabu hiyo.

Klabu ya Barcelona imetoka kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa msimu wa pili mfululizo jambo ambalo sio la kawaida kwa timu hiyo na mwaka huu timu imetolewa chini ya kocha Xavi na kuibua mijadala kua kocha huyo atafukuzwa klabuni hapo.laportaKlabu ya Barcelona mpaka wakati huu inaongoza msimamo wa ligi kuu nchini Hispania La liga kwa tofauti ya alama mbili wakiwa na alama 37 huku wapinzani wao Real Madrid wakiwa na alama 35.

aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa