Moratta Kubaki Atletico Madrid

Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid na timu ya taifa ya Hispania Alvaro Moratta ameweka wazi ataendelea kusalia ndani ya viunga vya Wanda Metropolitano.

Mshambuliaji Moratta alikua anahusishwa na moja ya vilabu vinayopatikana nchini Saudia Arabia lakini yeye mwenyewe ameweka wazi kubaki ndani ya klabu hiyo zaidi, Kwani mchezaji huyo bado ana mkataba ndani ya timu hiyo ambao utatamatika mwaka 2027.morattaMshamabuliaji huyo inaelezwa amekataa ofa ya klabu moja kutoka nchini Saudia Arabia na kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake jijini Madrid, Mchezaji huyo ameonekana ana furaha kuendelea kuwepo kwenye klabu ya Atletico na jiji la Madrid ambapo ndio mahala ambapo amezaliwa.

Licha ya wachezaji wengi kukimbilia ligi kuu ya Saudia Arabia wakiwa wameshafanikiwa katika ligi za ushindani barani ulaya kwa mfano Moratta ambaye mpaka sasa ameshafanikiwa kushinda kila taji katika ngazi ya klabu kwenye vilabu kama Real Madrid, Atletico Madrid, Juventus, na klabu ya Chelsea lakini yeye ameonekana kuamini kua bado ana uwezo wa kuendelea kupambana barani ulaya.

Acha ujumbe