Moratta: Sijui kama Nitabaki Atletico

Nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya Hispania na mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid Alvaro Moratta ameweka wazi juu ya mustakabali wake na kusema bado hajajua kama atabaki ndani ya klabu hiyo.

Moratta anasema amepokea jumbe nyingi kutoka kwa watu wengi kutoka klabu ya Atletico Madrid lakini hajapokea ujumbe kutoka kwa kocha wake Diego Simeone, Mchezaji alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa kuhusiana na mustakabli wake juu ya kubakia ndani ya Atletico.morattaMshambuliaji huyo haikuishia hapo kwani alisema licha ya kutokutimiwa ujumbe wowote na kocha wake Simeone, Lakini alisema anamuelewa kocha huyo kwani angekua hana mpango wa kuendelea nae msimu ujao angeshamueleza mapema.

Mshambuliaji Alvaro Moratta ana mkataba ndani ya viunga vya Wanda Metropolitano mpaka mwaka 2027 hivo mchezaji huyo anaweza kuwepo sana klabuni hapo, Huku taarifa za kuondoka kwake ndani ya klabu hiyo zikiishia kuongelewa tu.

Acha ujumbe