Klabu ya Real Madrid ipo mawindoni kwajili kumuwinda beki wa kushoto wa klabu ya Fc Bayern Munich Alphonso Davies raia wa kimataifa wa Canada kwajili ya kwenda kukipiga klabuni hapo.
Real Madrid imekua haina beki wa kushoto wa kudumu na mwenye ubora mkubwa tangu kutimka kwa Marcelo, Hivo Alphonso Davies anaonekana kama mbadala sahihi wa Marcelo klabuni hapo.Beki Ferlan Mendy amekua akisumbuliwa na majeraha mara kwa mara tangu ajiunge klabuni hapo, Lakini vilevile inaonekana ni kama viatu vya Marcelo Viera kumpwaya hivo mabingwa hao wa zamani wa ulaya wanatafuta beki mwingine wa kushoto.
Taarifa kutoka nchini Ujerumani zinaeleza beki Alphonso Davies hana mpango wa kusaini mkataba mpya ndani ya klabu ya Bayern Munich, Hii ikiendelea kuchochea kwa kiwango tetesi za mchezaji huyo kujiunga na mabingwa wa muda wote barani ulaya.Real Madrid wako kwenye mpango wa kuboresha safu yao ya ulinzi haswa upande wa pembeni, Kwani ukiachana na Alphonso Davies lakini klabu hiyo pia inafukuzia saini ya beki wa kulia wa Chelsea Reece James kwajili ya kujua kuvaa viatu vya Dani Carvajal.