Simeone Afurahia kuwepo Atletico

Kocha wa klabu ya Atletico Madrid raia wa kimataifa wa Argentina Diego Simeone amesema anafurahia kuendelea kuitumikia klabu hiyo na kuendelea kuwepo klabuni hapo kwa muda mrefu zaidi.

Simeone ameweka wazi kua ataendelea kukaka muda mrefu klabuni hapo na kuendelea kuuimarisha klabuni hiyo kwa miaka mingi zaidi, Kwani tangu kocha huyo ajiunge na klabu hiyo imekua ikifanya vizuri.simeoneKocha huyo amekua akipambana kuhakikisha klabu hiyo inafanya vizuri katika michuano mbalimbali, Lakini Diego amesema anafurahia kila siku kuona maendeleo ya klabu hiyo na inavyokua haswa kwenye michuano ya ulaya.

Raia huyo wa kimataifa wa Argentina amesema ni changamoto kwelikweli kuifanya Atletico Madrid kukua barani ulaya kila mwaka na ndio malengo yangu jambo ambalo linaonekana kua ndio mipango mikubwa ya kocha huyo.simeoneKocha Diego Simeone licha ya kuonekana kutamani kuifanya klabu ya Atletico Madrid kufanya vizuri barani ulaya, Lakini ameshafanikiwa kuifanya klabu hiyo kufika fainali ya michuano hiyo mara mbili na deni kubwa lililobaki inaonekana ni kutwaa taji hilo.

Acha ujumbe