Kagera Sugar Wayatimba Huko kwa Simba SC

simba

BAADA ya mastaa wa Simba kuyeyusha dakika 450 katika mechi tano za ushindani bila kushinda wanawafuata Kagera Sugar wakiwa wanabebwa na mambo makubwa matatu wanayoamini yatawapa ushindi.

Ipo wazi kuwa katika mechi tano walizocheza Simba mara ya mwisho kushinda ilikuwa Simba 2-1 Ihefu mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, katika mechi tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika waliambulia sare mbili na walipoteza mchezo mmoja huku kwenye ligi wakiambulia sare moja na walipoteza Kariakoo Dabi, Simba 1-5 Yanga. Unaweza kubashiri mechi hii kupitia Meridianbet ikiwa na odds kubwa. BASHIRI HAPA.

Mchezo wao wa sita unatarajiwa kuchezwa Desemba 15 Uwanja wa Uhuru ambao utakuwa wa ligi dhidi ya Kagera Sugar iliyotoka kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kuna mambo zaidi ya matatu katika kikosi hicho ikiwa ni ari kubwa ya wachezaji katika kikosi hicho, juhudi na kujiamini kwenye kutafuta ushindi katika mechi zinazofuata.

“Hatujapata matokeo mazuri kwenye mechi zetu zilizopita lakini kwa sasa kuna mambo mengi yameongeza ikiwa ni ari ya wachezaji ukiangalia kabisa unaona namna wachezaji wanavyojituma kutimiza majukumu yao.

“Pili ni juhudi kila mmoja anaonesha namna gani kuna kiu kubwa ya kupata ushindi jambo lingine ni ari mpya katika kikosi mapambano bado yanaendelea mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” alisema Ally.

Unaweza kuchagua machaguo tofauti zaidi ya 1000+ kwenye mechi hii pale MERIDIANBET kisha ubeti kupitia duka la ubashiri au mtandaoni.

Acha ujumbe