Tchouameni Nje Miezi Miwili

Kiungo wa klabu ya Real Madrid Aurelien Tchouameni anatarajia kukaa nje ya uwanja kwa takribani wiki sita mpaka nane kutokana na majeraha ambayo ameyapata katika mchezo wa jana dhidi ya Barcelona.

Kiungo Tchouameni amegundulika kupata majeraha katika mguu wake wa kushoto hivo madaktari wa klabu hiyo wamethibisha majeraha hayo yatamueka nje ya uwanja kwa wiki sita mpaka nane.TchouameniKiungo huyo mfaransa amekua kwenye kiwango bora sana msimu huu ndani ya klabu ya Real Madrid, Kwani klabu hiyo haijapoteza mchezo hata mmoja mpaka sasa ambao kiungo huyo ameanza msimu huu.

Klabu ya Real Madrid wanaweza kurudi kuanza na wakongwe Toni Kroos na Luca Modric katika michezo yao kutokana na majeraha ya kiungo huyo wa kimatiafa wa Ufaransa,Kwani yeye ndio alikua anaaanza muda mwingi msimu huu kwenye nafasi hiyo.TchouameniKiungo Tchouameni alipata majeraha baada ya michuano ya kombe la dunia mwaka jana ambayo yalimueka nje ya uwanja kwa muda mrefu na kupelekea kupoteza nafasi yake klabuni hapo, Hivo majeraha yake hayana ishara nzuri kwani anaweza kuja kufanya kazi kubwa ya kuirudisha nafasi yake akitoka kwenye majeraha.

Acha ujumbe