Yamal Atamani Kucheza na Nico Williams Barca

Kinda wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Lamine Yamal amezungumza juu ya mchezaji ambaye anatamani kucheza nae akimtaja winga wa klabu ya Atletic Bilbao Nico Williams.

Yamal amesema angepata nafasi ya kusajili mchezaji mmoja kwenye kikosi cha Barcelona basi mchezaji wa kwanza angekua ni Nico Williams ambaye amekua akifanya vizuri kwenye klabu ya Athletic Bilbao pamoja na kikosi cha timu ya taifa ya Hispania maarufu kama La Roja.yamalWinga huyo wa klabu ya Barcelona amekua na ukaribu mkubwa sana na Nico Williams jambo ambalo limefanya kutaka kucheza nae ndani ya klabu ya Barcelona, Lakini uwezo pia umekua ni moja ya nguzo ambayo imemfanya Lmaine kutamani kucheza na Nico.

Klabu ya Barcelona pia inaelezwa kua inamfukuzia winga huyo kutoka klabu ya Atletic Bilbao jambo ambalo linaweza kutimiza ndoto ya Lamine Yamal, Kwani anaona ushirikiano wao ndani ya klabu ya Barcelona unaweza kua wenye kutisha na kuipa mafanikio makubwa klabu ya Barcelona.

Acha ujumbe