Cancelo: Napenda Kuendelea Kubaki Barcelona

Beki wa klabu ya Manchester City anayekipiga ndani ya klabu ya Barcelona kwa mkopo Joao Cancelo ameweka wazi anapendelea kubaki ndani ya klabu ya Barcelona kwa muda mrefu zaidi.

Cancelo mara kadhaa amekua akionesha kua anahitaji kubaki ndani ya klabu ya Barcelona licha ya kua kuitumikia klabu hiyo kwa mkopo, Hivo kinachosubiriwa hapo ni makubaliano baina ya klabu ya Man City na Barcelona ili kuamua hatma ya beki huyo wa kimataifa wa Ureno.canceloBeki huyo amekua akionesha kiwango bora ndani ya klabu ya Barcelona jambo ambalo pia limemfanya Rais wa klabu hiyo Joan Laporta kufikiria kumbakiza ndani ya timu hiyo, Huku pia amesikika mara kwa mara kua mipango yao ni kumbakiza beki huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi tofauti tofauti uwanjani.

Mara kadhaa kocha Josep Guardiola amesikika akizungumza juu ya beki Joao Cancelo na kusema kua bado ni mchezaji wao, Hivo kama klabu ya Barcelona wanapaswa kukaa mezani na Man City na kuweka dau ambalo wamiliki wa mchezaji wataliridhia ikishindikana ni wazi mchezaji huyo atarudi kwenye klabu yake.

Acha ujumbe