Rabiot Hajui Hatma Yake Juventus

Kiungo wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa Andrien Rabiot bado hajajua hatma yake ndani ya klabu ya Juventus ambapo mpaka sasa amebakiza siku 10 mkataba wake umalizike ndani ya timu hiyo.

Rabiot amezungumza juu ya mustakabali wake ndani ya timu hiyo pamoja na ujio wa kocha mpya klabuni hapo ambaye alikua mchezaji mwenzake ndani ya klabu ya PSG Thiago Motta “Yeye ni meneja bora sana, alifanya kazi nzuri sana huko Bologna. Tulikuwa tukicheza pamoja PSG.”rabiot“Thiago ana kazi yake mwenyewe, mimi nina yangu… kwa hiyo tutaona. Lakini Juve wamechagua vizuri kwa kumchagua Thiago Motta.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa ni wazi bado hajajua mustakabali wake ndani ya klabu ya Juventus kutokana na maelezo ambayo ameyatoa, Mpaka sasa Rabiot hajajua kama ataendelea kusalia ndnai ya viunga vya Turin au atatimka klabuni hapo baada ya kukaa takribani misimu miwili.

Acha ujumbe