Ni kizungumkuti linapokuja suala la usajili ndani ya Manchester United. Baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wameanza kuonesha hisia zinazokinzana kwenye usajili.
Ni kawaida ya Man United kuhusishwa na wachezaji wa kila kariba, kwa mazingira ya sasa – Frankie De Jong na Darwin Nunez ni wachezaji wanaotajwa zaidi kule Old Trafford pamoja na miongoni mwa mashabiki na vyombo vya habari.
Kinachoonekana machoni na kusikika masikioni mwa watu ni kuwa, De Jong hataki kuondoka Barca na, ikitokea ameondoka, basi ataenda kwenye timu inayocheza UEFA (hapa The Red Devils wameshafeli). Fumba na kufumbua, Liverpool wameingia miguu yote kwenye usajili wa Nunez akitazamwa kama mbadala wa Mane anayehusishwa na Bayern.

Kwa hali ilivyo, kumezuka hali ya sintofahamu huku baadhi ya mashabiki wa M16 wakipaza sauti zao kupitia mitandao ya kijamii. Mjadala mkubwa umekuwa ni kipi muhimu kwa timu hiyo – ni kumsajili mshambuliaji (CF) au kiungo (CM). Sintofahamu ya kipaumbele cha timu hiyo, kinawagawa mashabiki.
Wapo wanaokereketwa na uwezekano wa United kuwakosa De Jong na Nunez kwa pamoja, wapo wanaokerekwa zaidi na uhalisia wa timu hiyo kuhusishwa na Nunez kwa muda mrefu na sasa, wanaelekea kupokonywa tonge mdomoni na Liverpool. Wapo wanaodhani ni kupoteza muda kwa klabu kama Manchester kumlazimisha De Jong kuja wakati hataki.

Dirisha la usajili linafunguliwa rasmi saa 6 kamili leo usiku, pengine kuna mengi zaidi yataonekana kuelekea msimu ujao, 2022/23.
ALIYA’S WISHES
Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.