Makamu wa rais wa klabu ya Barcelona amekubali kuwa klabu hiyo inauhitaji wa kiasi cha €500milioni ili kuinusuru klabu hiyo kutoka kwenye mdororo wa kiuchumi ambao unaukabili.

Barcelona kwa sasa kutokana na ukomo wa matumizi ya mapato haiwezi kusajiri mchezaji yoyote, ikiwa watataka kumsajiri mchezaji mpya itawabidi wauze wachezaji ili kutoa nafasi ya wachezaji wapya kwa sasa.

Barcelona

Barcelona kwa sasa inahitaji kiasi cha €500milioni ili kuweza kuongeza mtaji wa uendeshaji wa klabu hiyo kwa msimu unaotarajiwa kuanza mwezi Agosti. Tayari raisi wa klabu hiyo Joan Laporta ashaanza mikakati ya kutaka kuikomboa klabu hiyo kwa kutaka kuuza hatimiliki za haki ya matangazo ya Radio ili kuweza kupata pesa.

Mpaka sasa klabu hiyo ishapeleka mapendekezo kadhaa ya kuuza hati miliki zake mbalimbali kwenye bodi ya klabu, ikiwemo hati miliki za matangazo ya Tv, radio na matangazo ili kufanikisha kupata kiasi kinachokadiriwa kuwa €700 na zaidi.

Japokuwa klabu ya Barcelona inauhitaji mkubwa wa fedha lakini bado wamekuwa na mashaka na na kampuni ya CVC, ambayo inapigiwa chapuo na La Liga kwenye hati za matangazo ya television ambapo klabu hiyo itaingiza kiasi kikubwa .


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa