Kwa mujibu wa Jorge Mendes, wakala anayetajwa kuwa mmoja wa mawakala wenye ushawishi mkubwa duniani, staa wa Barcelona Nico Gonzalez atasalia klabuni hapo.
Jorge Mendes: Nico Gonzalez
Nico Gonzalez

Jorge Mendes alikutana na Wakurugenzi wa Barcelona na kujadili mambo kadhaa kwa muda wa takribani masaa mawili na nusu.

Kwa mujibu wa Mundo Deportivo, Jorge Mendes alikutana na Mkurugenzi wa Michezo Mateu Alemany na Mtendaji wa Ufundi Jordi Cruffy.

Kufuatia uwepo wa taarifa za Nico kuhusishwa na kuondoka klabuni hapo, wakala huyu alinukuliwa akisema;

“Nico Gonzalez hawataki kumuuza, hata wakipewa ofa kwa ajili yake, atabaki. Lakini tulizungumza juu ya wachezaji wengine na kila kitu kilienda vyema.” – Jorge Mendes

 

Jorge Mendes: Nico Gonzalez

Taarifa hizi zinaashiria kuwa Xavi amepania kumtumia vyema staa huyu mwenye miaka 20 kuelekea msimu ujao.

Jorge Mendes ni wakala anayewawakilisha wachezaji kadhaa na inaaminika kikao hiki kilikuwa na mazungumzo juu ya Angel di Maria, Ruben Neves na Goncalo Guedes. Hali ya sasa ya Francisco Trincao na Adama Traore inatajwa kuwa huenda nayo ikawa imezungumziwa.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa. Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa