Mchezaji wa PSG Kylian Mbappe amekubali kuwa klabu yake PSG haikufanya vya kutosha ili waongoze kundi lao la Ligi ya Mabingwa, ambalo Benfica waliweza kuongoza baada ya kuitandika Maccabi mabao sita kwa moja.

Mabao kutoka kwa Mbappe na Nuno Mendes wakiwa Turin hayakutosha kwa wao kuongoza kundi hilo huku Juventus wao wakiambulia bao moja kupitia kwa mchezaji wao Leonard Bonucci, Lakini vijana hao wa Christophe Galtier waliishia nafasi ya pili baada ya ushindi wa 2-1.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Ligi ya Mabingwa, PSG na Benfica hazikuweza kutenganishwa na rekodi yao ya kufungana, kufunga au kufungwa, ingawa Mbappe alipendekeza timu yake ingefanya zaidi.

Mbappe alisema kuwa wakati wa mechi hawakujua, lakini mwishowe walijaribu kuwaonya, lakini huo ulikuwa mwisho, haijalishi kama tulifuzu ila tulikuja kufanya kazi na hiyo haitoshi tutaangalia sare au tutacheza kushinda.
Galtier alibainisha ushindi wa PSG wa 7-2 dhidi ya Maccabi katika mechi yao ya 5 kama ishara ya onyo na alisikitikia matokeo mazuri ambayo yaliifanya timu yake kumaliza nafasi ya pili. Alisema kuwa;
“Tuliposhinda 7-2 wiki iliyopita, tuliacha kucheza dakika ya 90 na tuliruhusu mabao mengi sana wakati wa hatua ya makundi kutoka kwenye timu kadhaa, kama tulivyofanya dhidi ya Maccabi na kama tungeruhusu bao moja pungufu, tungekuwa tumemaliza tukiwa juu ya kundi.”

PSG imeshindwa kuongoza kundi lao la Ligi ya Mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kumaliza katika nafasi ya kwanza katika kila mechi kati ya nne zilizopita, lakini Galtier alisisitiza kuwa kikosi chake bado kimefanya vyema katika michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.
Galtier alimaliza kwa kuipongeza timu yake kwa hapo ilipofikia na kusema kuwa wamefanya vizuri lakini pia aliwapongeza Benfica kwa kuonyesha kiwango kizuri na pia kufurahia kuifunga Juventus mara mbili.
Sasa kilichobaki ni kusubiria droo tu ipangwe katika hatua hiyo waliyofikia katika mashindano hayo, na lazima ushinde timu kubwa ndio utaweza kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hii.


