Klabu ya soka ya Manchester United itampatia kipaumbele mchezaji beki wa kushoto wa klabu ya Juventus na Brazil, Alex Sandro ambaye ana miaka 27 kubeba nafasi ya mchezaji beki wa kushoto wa huko Uingereza mwenye umri wa miaka 22, Luke Shaw.
Wanataraji kufanya hivyo ifikapo msimu ujao na kuwa kwa sasa pia kocha wao Jose Mourinho yupo tayari kumchezesha Anthony Martial kwenye safu ya kati ya mashambulizi msimu ujao. Ila hili litafanyika endapo tu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atabakia klabuni hapo.


Povel
Habar njema