Mshambuliaji wa Juventus, Cristano Ronaldo anaripotiwa kuwa chini ya uchunguzi kufuatia ushangiliaji wake mpya kwenye gemu dhidi ya Atletico Madrid ambayo alichapa magoli matatu na kuisaidia klabu yake kuingia hatua ya robo fainali.
Ronaldo alikuwa shujaa wa alikuwa Shujaa wa Juventus, baada ya kuondoa gepu la 2-0 la kwenye mzunguko wa kwanza kwenye hatua ya mtoano wa klabu 16, Magoli yake matatu yalikuwa ni kila kitu walichokihitaji Juve kuingia robo fainali.
Goli la tatu la staa huyu lilipatikana kwa mkwaju wa penati, na baada ya kuchapa goli hilo alikimbia na kushangilia tufauti na anavyoshangilia wakati wote, hapa aliongeza mbwembwe na alishangilia mbele ya mashabiki wa Atletico akimuiga Diego Simione alivyoshangilia kwenye gemu ya kwanza. Hata hivyo staili aliyoitumia staa huyu inatafsiriwa kuwa kama aliwatukana mashabiki wa Atletico.

Taarifa zianadai UEFA wanafanya uchunguzi kufuatia aina hiyo ya ushangiliaji. Huenda staa huyu akakutana na adhabu. Inahofiwa kuwa huenda akakosa gemu moja au zote 2 za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya au akalipishwa tu faini inategemea na maamuzi yatakayotolewa.
Diego Simione, meneja wa Atletico ambaye alishangilia hivyo kwa mara ya kwanza alikutana na rungu la UEFA na kutakiwa kulipa faini ya paundi 20,000, hivyo huenda Ronaldo akapewa adhabu sawa na hiyo.


Povel
Gud news
Fatina mfingi
Mmh!!
Gabriel
Good news 👍