Baada ya PSG, Tunanyoka na Barca -Ole Gunnar

Ole Gunnar anaamini vijana wake wanaweza wakatoboa moja kwa moja kwenye hatua ya nusu fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya droo kuwapa Barcelona kama mpinzani wao kwenye hatua ya robo fainali.

Baada ya droo hii, meneja huyu anakuwa anarejea Nou Camp baada ya miaka 20 toka alipochapa bao la ushindi mwaka 1999 kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa.

United wanatarajia kukutana na wababe wao kwenye Ligi Kuu -EPL Liverpool kwenye hatua ya nusu fainali kama wote watafanikiwa kutoboa kwenye hatua ya robo fainali.

Ole Gunnar anasema kwa soka ambalo walichapa dhidi ya PSG, ambapo waliweza kupindua matokeo waliyopata kwenye mzunguko wa kwanza ya 2-0 na kushinda 3-1 ugenini na kujikuta wametoboa kuingia robo fainali waliionesha dunia kuwa wana uwezo wa kuichapa klabu yeyote kubwa.

Robo fainali dhidi ya Barcelona ndio wakati muafaka wa Ole Gunnar Kuonesha ubora wake na namna anavyoweza kuwachezesha vijana wake kwenda sawa kasi ya Barcelona na hatimaye kuingia hatua inayofuta. Bila shaka atakuwa anajiweka karibu zaidi na kibarua cha kudumu klabuni hapo.

Hata hivyo, licha ya imani aliyonayo juu ya kikosi chake bado anatambua ukweli kuwa kuna ushindani mkubwa kwenye ligi hii.

“Kila timu inaweza kumpiga yeyote kati ya hizi nane. Lakini badao zipo timu bora zaidi.”
“Nafikiri tumeonesha dhidi ya PSG kuwa siku yeyote tunaweza kuwachapa timu yeyote kubwa.”

-Ole Gunnar

3 Komentara

    Mliwaweza psg sio barca hapo united msahau

    Jibu

    Habar njema sana 👍

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe