Alexis Sanchez yupo tayari kuendelea kusalia OT kupigania namba yake chini ya kikosi hicho kinachoendelea kusukwa kwa sasa. Pamoja na kwamba matajiri wa klabu hiyo wanatamani endapo mchezaji huyo kama anaendelea kusuasua na kiwango chake ni vyema akaongoka ili kupunguza gharama za kiuendeshaji na mshahara mkubwa anaoupokea kwa sasa.
Sanchez alijiunga na klabu hiyo akitokea Arsenal mapema Januari katika biashara iliyokuwa ya mbadilishano kati yake na Henrikh Mkhitaryan ambao walipishana na kila mmoja aliondoka akiwa anatamani kwa nafasi fulani kutemana na klabu yake ya mwanzo kutokana na kunyimwa nafasi za kutosha uwanjani. Japo Sanchez aliondoka akiwa na nia ya kuachana na Arsenal alichokiona yeye kama ukosefu wa mataji makubwa.
Raia huyo wa Chile hajawa na msimu mzuri kabisa ndani ya kikosi hicho baada ya kufanikiwa kufunga goli moja tu msimu huu lakini kwa upande wa pili akiwa ni mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa sana wa £500,000 kitu ambacho anapaswa kuwalipa United fadhila za kile wanachokiamini kwake.
United walimwiba mchezaji huyo mdomoni kabisa mwa wapinzani wao Manchester City kama inavyokumbukwa kwamba mchezaji huyo alikuwa karibu kujiunga na miamba hao lakini malengo yake yalikatika ghafla baada ya United kuonesha nia ya wazi kabisa kumsajili mchezaji huyo mapema sana.
Kama ilivyo kwa sasa klabu hiyo ipo katika mwenendo wa kumkabidhi mkataba wa kudumu Ole Gunnar awe kocha mkuu ndani ya kikosi hicho kutokana na matunda aliyoyaonesha mapema sana baada ya kuilea timu hiyo. Kutokana na hilo United wanatamani kuweka vizuri suala la mishahara ya wachezaji kusudi kuhakikisha vitabu vyao vinabaki salama.
Pamoja na matamanio hayo ya United kumuuza lakini kwake Sanchez hayupo tayari kuondoka na anachotazamia zaidi ni kuendelea kusalia kikosini hapo kwa kipindi kingine na zaidi anatazamia kuleta mabadiliko katika kipindi kijacho pamoja na kwamba hajapata utulivu wa kutosha kikosini.
Kumekuwa na matamanio mbalimbali kutoka kwa klabu nyingine kubwa kama PSG na klabu nyingine za Hispania lakini suala la mshahara anaopokea mchezaji huyo bado linaonekana kuwa kikwazo kwake kujiunga na klabu nyingine maana wanaonelea inaweza kuwaletea ugumu kukidhi haja za mchezaji huyo anayekula donge nono.
Uwepo wa Sanchez na aina ya malipo anayopokea kwa sasa yanaonekana kuwa na athari kwani hata mlinda mlango wa kikosi hicho, David De Gea ameanza kuomba kupandishiwa mshahara wake kutokana na mwenzake kuonekana analipwa kiwango hicho. Jambo hilo linaonekana kuchochewa na malipo ya awali yanayopokelewa na Sanchez, hicho ni kitu kinachofanya makubaliano ya De Gea kushindwa kuafikiwa kwa wakati.


Isha
Safi sana ametisha sana
Povel
Gud news
Furahav
Noma sana.
Issa
Habari nzuri