Mlinzi wa kushoto wa klabu ya Real Madrid anahusishwa na kujiunga na klabu ya Juventus kwa kipindi cha hivi karibuni baada ya kupoteza kabisa nafasi ya kuanza ndani ya kikosi cha Zidane kilichopotea sana ndani ya ligi na michuano mingine ya kimataifa ambayo klabu hiyo inashiriki kwa sasa.
Klabu hiyo kwa sasa imeonekana kutompa nafasi kabisa ya kucheza mlinzi huyo ambaye ni mkongwe ndani ya klabu hiyo ambaye kwa kiwango kikubwa amehusika na mafanikio makubwa ya klabu hiyo. Lakini mwalimu aliyepita wa klabu hiyo alikosa kabisa nia ya dhati ya kumtumia mchezaji huyo ndani ya kikosi chake kutokana na sababu za kimfumo.
Huu ukiwa ni msimu wake wa 13 ndani ya klabu hiyo lakini Solari alionekana kutohitaji huduma yake na akapendelea kumtumia sana Sergio Reguilon katika safu yake walinzi hususan upande wa kushoto kitu kinachomfanya Marcelo aendelee kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.
Ripoti hizi zinaweza zisiwe mpya sana kwa upande wa mashabiki wa Juventus kutokana na kwamba aliwahi kuhusishwa mara kadhaa kujiunga na miamba hao wa soka nchini Italia na kwa taarifa za awali tayari kuna maafikiano ya awali yameweza kufikiwa baina yao na kwamba mchezaji huyo wakati wowote wa usajili ataweza kujiunga nao.

Marcelo amekubaliana nao kusaini mkataba wa kuwa klabuni hapo kwa muda usiopungua miaka minne huku akiwa anapokea kiasi cha €12M kwa msimu. Na akipokea kiwango hicho ni kikubwa sana katika hali ya kawaida kwa mchezaji kuvuna na ni hakika Marcelo asingeweza kuendelea kusalia hapo kutokana na hali hiyo.
Juventus wanaonekana kuwa na lengo kubwa kibiashara msimu huu kutokana pia na taarifa zao za kuendelea kumuwinda Isco ambaye waliwahi kumuweka kwenye kilengeo chao na kama wangeweza kumpata kwa siku za usoni ili kuweka mahusiano ya karibu kujadili kama angeweza kujiunga nao maana naye hajapata wakati mwingi wa kuweza kucheza chini ya Solari.
Safari ya Marcelo kwenda Juventus itaweza kumuunganisha na Ronaldo kwa sasa baada ya ile miaka tisa ya kuwa pamoja ndani ya jiji la Hispania na isitoshe wawili hao walikuwa ni marafiki wa karibu sana na hata kuondoka kwa Ronaldo kulionekana kabisa kutompendeza Marcelo. Hivyo muunganiko wao ni sehemu kubwa ya mafanikio kwao.
Ukaribu wa wawili hao ulikuwa mzuri mpaka ikafika wakati wakawa wanaambizana siri na hata safari ya Ronaldo kwenda Juventus Marcelo aliijua mapema sana wakati wakiwa mazoezini kuikabili Liverpool.
Marcelo alisaini mkataba wake 2017 ambao utaisha 2022 lakini kwa sasa anaelekea kubadili maamuzi yake kutokana na hali anayoielezea kwamba hana nafasi tena ndani ya kikosi hicho na kwa sasa hafurahishwi tena na maisha ya hapo kutokana.

