Kunako Michuano ya Europa, mchezo wa Manchester United dhidi ya Sevilla katika hatua ya nusu fainali unatizamwa kipee na Robin Van Persie.
Baada ya kuwagaragaza FC Copenhagen katika hatua ya robo fainali, Man United sasa watamenyana na Sevilla ambao waliwaburuza Wolves katika hatua ya robo fainali. Huu ni mchezo wa aina yake katika kutafuta tiketi ya kucheza fainali ya Ligi ya Europa wiki ijayo.

Akizungumza na Stats Platform News, Van Persie amesema ” Sevilla ni kati ya timu zenye nafasi ya ubingwa lakini wanapaswa kuitafuta kupitia Man United. Ni wapambanaji wa makombe na wamekuwa wakifanya hivyo mara zote.”
“Ilikuwa bado kidogo nifanye nao mazungumzo kabla sijajiunga na Arsenal (2004), ilikuwa ni moja kati ya timu tatu ambazo ningeweza kujiunga nao. Ilikuwa inanishawishi kwenda Sevilla lakini niliamua kuichagua Arsenal.”

Sevilla wamewahi kubeba Kombe la Europa mara 5, mara mbili kipindi kombe hilo [Europa] likijulikana kama UEFA Cup na mara 3 mfululizo kuanzia mwaka 2014-2016. Hii ni moja ya sababu ambayo Van Persie anaiona kama ni angalizo wa Ole Gunnar Solskjaer.
Man United wamemaliza msimu wakiwa katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa EPL msimu huu na kuwapa tiketi ya kushiriki michuano ya UEFA msimu ujao. Wakiwa na rekodi ya kupoteza michezo miwili ya nusu fainali msimu huu, Van Persie amesema;

“miezi kadhaa iliyopita [Man United] wameonesha uwezo chanya lakini wanapaswa kuonesha uwezo huohuo katika michuano hii. Siwezi kusema kwamba wasiposhinda basi hawajafanikiwa kitu msimu, La hasha! baada ya mapumziko (ya Corona) wameonesha uwezo mkubwa na jambo jema kuelekea msimu ujao.”
Robin Van Persie alikuwa mchezaji wa Manchester United na alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza – EPL mwaka 2012/2013, hiyo ndiyo mara ya mwisho kwa Manchester United kubeba ubingwa wa EPL mpaka sasa.
Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.


lombo
mambo ni moto na meridianbet
Furahav
Van persie yuko sahii,mana sevila nao wako vizuri.
Hope mwaikuka
Tx for news
Dorophina
Ni kweli maneno yake lkn wakumbuke mchezo hautabiliki lolote linaweza kutokea kwenye mchezo
warda
Van persie anaiwazia timu yake jamani#Meridianbettz
Devotha
Itabidi wajipange haswaa man United maana Sevilla sio timu ya mchezomchezo
Sadick
Tahadhari ya mkongwe Van Persie ni sahihi hasa nikizingatia kiwango duni wachoonyesha Man U mechi yake na dhidi ya Copenhagen#meridianbettz
Povel
Yap ni Jambo zuri kumuheshimu mpnzan wako kila la kheri man United kpnz cha wengi
Shafii
Van persie yuko sahihi sevilla ndiye bingwa Mara nyingi wa kombe hilo inapaswa ajipangee.
Gabriel
Hii mechi kal sana 👍
Fatuma kasomo
Sevila ndio bingwa mara zote wakombe hilo
Asia Abdy
Nice👏
Latifa juma mohamed
Ahsanteni kwa kutujuza haya
Salma ngende
Mechi kali
Issa
Man u watafika fainal sevilla hawana historia mbele ya man
Omary lukumbi
Jambo ni shabiki mkubwa wa man united lakin haipaswi united kuidharau Sevilla kwenye michuano hii kikubwa kucheza soka la nguvu na kua makin dakika zote 90
Ester jackson
Kweli kabisa kwa hasaivi inatajiwa kila timu kuiheshimu mpizani wake kusubiri matokeo mana sasa yunaona ambao hawatabiriki kushinda sasa wanashinda .
Rose kapinga
Heshimaa lazima iwepo!!!
Mwajumah
Hii mechi kali sana#Meridianbettz
Adelta
👏👏@meridianbettz
aisha
Hii mechi ni yakibabe sana
Zeiyana
Man Chester utd ya sasa si ile ya zamani kwa watokea waliyo kua nayo sijui kama wataweza kweli..!mabingwa wanajulikana
Mwanahamisi
Hii mechi ya kibabe
Fatina mfingi
Mechi kali hatar
Sabrina
Huu mtanange utakua hatari hii mechi sio ya kukosa.
Lydia Emmanuel Magoti
Namuwerewa Van Persie kitambo anajua jembe hilo
felister
lolote linaweza kutokea mpira dk 90
Caroline
Ni kweli Sevilla wapo vizuri
Tatu
Man wanatakiwa kujipanga sawasawa
Ernest
Salute kwa Van Persie maana ameongea kitu cha kuwafanya wachezaji wa Man U kuwa macho zaidi
Njiku
Sevilla timu bora Sana’a na kubwa sana hasa kwa kombe la uropa wanahistoria nzuri sana na kombe hilo man wanatakiwa waende kupambana
Samiah
👏👏👏👏
Saupha mohamed
Good news
Janeflora malisa
Nice
farida ahmadi
Yuko sahihi kabisah lolote linaweza kutokea
David Pere
Baada ya kuwagaragaza FC Copenhagen katika hatua ya robo fainali, Man United sasa watamenyana na Sevilla ambao waliwaburuza Wolves katika hatua ya robo fainali. Huu ni mchezo wa aina yake katika kutafuta tiketi ya kucheza fainali ya Ligi ya Europa wiki ijayo.
magdalena
sevilla tutaipa heshima sababu ilitufunga hatuna namna
Shan
Mwisho wa dk 90 man u out.