Kristiano Ronaldo na Lionel Messi wanamchango mkubwa sana kwenye soka na rekodi ambazo ni ngumu sana kufikiwa katika miaka ya 2010, na hakuna hata anae karibia rekodi zao. lakini Ronaldo na Messy hawatabaki milele, Je ni nani atakae ziba au kujaza nafasi zilizo achwa na Magwiji hao?
Hapa tutakuletea baadhi na tungependa kuona mapenekezo yako hapo chini kwenye kuchangia unadhani ni nani atachukua nafasi ya wawili hao.
Kylian Mbappe (Paris St-Germain na Timu ya taifa ya Ufaransa)

Mbape amezaliwa tarehe 20 mwezi Disemba mwaka 1998 na ni mshambuliaji, anamiaka 21 pekee lakini tayari ana Kombe la dunia aliloshinda na timu ya taifa ya Ufaransa lililofanyika Nchini Urusi mwaka 2018 na bila kupepesa macho mbape ni moja ya wanasoka wenye uwezo mkubwa sana na umri mdogo.

Joao Felix (Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ureno)

Joao Felix amezaliwa tarehe 10 mwezi wa kumi na moja na kwasasa anamiaka 20, Timu ya Atretico Madrid imetumia zaidi ya pauni milioni 113 kumnunua Felix kutoka Benfica mwezi Julai. na akaweka rekodi ya kua mwanasoka wa tatu kwa kununuliwa kwa thamani kubwa Duniani kwa kijana Baro Baro aliyecheza mechi 43 tu kwenye kikosi cha kwanza cha Benfica.
Jadon Sancho (Borussia Dortmund na timu ya taifa la Uingeleza)

Jadon Sancho amezaliwa tarehe 25 mwezi Machi na tumemuweka kwenye list ya wakali hawa kwasababu ya kazi anayoifanya pale Dortmund. Nimeona mechi nyingi alizocheza na sina shaka na uwezo wake wa kusababisha magoli na kufunga lakini kubwa kuliko vyote uwezo wake wa kujiamini.
Ansu Fati (Barcelona na Timu ya taifa la Uhispania chini ya 21)

Ansu Fati amezaliwa tarehe 30 mwezi Oktoba mwaka 2002, ni mshambuliaji mwenye kasi kama umeme anapokua na mpira, Uwezo wake wa kutereza na mpira na bila kuupoteza mguuni kwake, Historia ya kinda huyu mwenye miaka 17 tu inaweza kutumika hata kwenye movie za hollywood.
Trent Alexander-Arnold (Liverpool na timu ya taifa ya Uingeleza)

Alexander-Arnoldamezaliwa tarehe 7 Okoba mwaka 1998, Liverpool imepata mchezaji waajabu sana anae weza kucheza nadasi zote kama Beki na wakati huo huo kama mshambuliaji wa kuhofiwa pindi wanapokutana na timu pinzani.
Mason Greenwood (Manchester United & England U21)

Greenwood amekua moja wa Makinda waliojizolea umaarufu mkubwa na Kikosi cha kwanza cha Manchester United akiwa na Umri wa miaka 19 tu. Wachezaji wengi wanapo pata nafasi za kucheza kwenye vikosi vya timu kubwa huchelewa kidogo kwenda sambamba na kasi ya timu zao lakini kwa Greenwood ni tofauti, anaonekana kujipanga na ni mbaya sana anapokua langoni mwa timu pinzani.
Hawa ni wachache sana kati wengi wanao paswa kuatazamwa kwa uangalifu sana hususan katika dhima nzima ya kufikia rekodi za kaka zao.


Issa
Wakali tu hawa