Mshambuliaji wa United Odion Ighalo anaonya kuwa EPL bado haijatambua vyema makali ya Bruno Fernandes!
Fernandes amekuwa akiwafurahisha United tangu alipofika klabuni hapo akitokea Sporting Lisbon. Ameanza maisha yake Uingereza kwa kupeta EPL kabla ya ligi kusimama kwa ajili ya maambukizi ya virusi vya corona.

Ighalo yeye amefika kwa mkopo klabuni hapo, naye aameanza vyema kuchapa kazi United akifurahia kucheza pamoja na Fernandes. Ighalo amemwagia sifa Fernandez na kusema kuwa anatarajia nyota huyo ataonesha maajabu zadi EPL.
“Bruno ni mchezaji mzuri, nilicheza naye nilipokuwa Udinese mwaka 3013/14. Bado hatujaona makali yake zaidi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza” -Odion
Ighalo anaamini baada ya Fernandes kutulizana Uingereza, basi atawaonesha nini anaweze kukifanya kwenye Ligi ya Primia.
Huenda ana mfahamu vyema kupitia uzoefu aliokuwa nao pindi wawili hawa walipokuwa klabu moja. Amemwaga sifa kibao juu ya uwezo wake wa kutafuta mpira, kuona goli na kuchapa magoli mengi.
Ni suala la muda kuona ukweli wa hiki anachokisema!


Rehema Dickson
Na bado yuko vizuri ata sasa