KLABU ya Barcelona inayocheza ligi kuu ya nchini Hispania imeripotiwa kuvutiwa na mchezaji wa taifa la Ghana Mohamed Kudus (22), ambaye amekuwa na kiwango kizuri sana tangua kuanza kwa michuano hii ya kombe la dunia nchini Qatar.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa juu wa Barcelona Jordi Cruyff ambaye ni Mkurugenzi wa Michezo, inaeleza kuwa wamekuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu sana Mohamed Kudus huku akiweka wazi kuwa anaivutia sana klabu hiyo.
“Tumekuwa tukimfuatilia Mohamed Kudus kwa zaidi ya mwaka, hatuweza kusema kwamba Barca wanamtaka Kudus lakini anavutia. Anafunga mabao na Holland wanazungumzia zaidi kuhusu nafasi yake, hivyo namjua mno yeye” Alisema Cruyff.
Barça director Cruyff: “We’ve been tracking Mohamed Kudus for more than one year. We can’t say now that Barça want Kudus… but he’s attracting interest”, told RAC 1. 🚨🔵🔴 #FCB
“He’s scoring goals and in Holland they discuss a lot about his position, so yes – I know him well”. pic.twitter.com/QjDmmYIrWp
— Fabrizio Romano (@FabrizioRomano) November 30, 2022
Mohamed Kudus anaichezea klabu ya Ajax kwenye nafasi ya kiungo wa kati, na amekuwa na mchango mkubwa pia hata kwenye timu yake ya taifa ya Ghana akiwa ameifungia mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Korea ambao walishinda kwa jumala ya 3-2.

Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

