Ecuador Yaanza Vyema Kombe la Dunia

Timu ya Taifa ya Ecuador imeanza vyema michuano hii ya Kombe la Dunia baada ya kuitungua kwa mabao 2-0 Qatar ambaye ndiye mwenyeji wa michuano hii nyumbani kwake katika uwanja wa Al Bayt.

 

Ecuador Yaanza Vyema Kombe la Dunia

Mabao hayo ya Ecuador yalitupiwa kimyani na mchezaji wao Enner Valencia katika kipindi cha kwanza cha mchezo kabla ya bao la dakika ya 3 kukataliwa na VAR.

Nahodha huyo anakuwa mfungaji bora wa Ecuador katika Kombe la Dunia akiwa na jumla ya mabao mawili na kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo wa kwanza wa ufunguzi wa michuano hii.

Qatar walionekana kuwa chini ya kiwango katika mechi yao ya kwanza kabisa ya Kombe la Dunia, wakishindwa hata kupiga shuti lililolenga lango huku wapinzani wao wakipiga mashuti matatu, na kuwafanya kuanza vyema kwenye Kundi A.

Ecuador Yaanza Vyema Kombe la Dunia

Valencia alitumia vyema makosa ya safu ya ulinzi ya Qatar na kuwaadhibu ipasavyo huku akiisadia nchi yake kuanza vyema kabisa. Lakini pia mchezaji huyo alihitaji matibabu ya jeraha la goti mwishoni mwa kipindi cha kwanza lakini aliendelea na mchezo.

Kutokana na Qatar kupoteza mechi hiyo sasa, inamaanisha kuwa wameingia katika Kombe lao la kwanza la Dunia wakiwa nje na mabingwa hao wa Asia walionyesha ni kwa nini wakiwa nchi mwenyeji wa kwanza kupoteza mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia.

Ecuador Yaanza Vyema Kombe la Dunia

Kikosi cha Gustavo Alfaro sasa kimecheza mechi saba mfululizo bila kupoteza, huku kukiwa na majaribio makubwa zaidi dhidi ya Uholanzi na Senegal.


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

 

Acha ujumbe