NAHODHA wa Klabu ya Simba John Raphael Bocco ni kama amewaumbua wale wote waliokuwa wakimsema na kumkosoa kwa kiwangao chake, hii ni baada ya kufunga Hattrick yake ya kwanza kwenye Ligi Kuu ya NBC, na kumfanya kuwa mchezaji wa pili kuweka rekodi hiyo baada ya Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele kufanya hivyo dhidi ya Singida BS.

 

bocco

Mchezo dhidi ya Ruvu Shooting umeng’arisha nyota ya Bocco kulingana na kiwango chake alichokionesha kuwa kizuri, na huenda ikawa ni mwanzo mzuri wa Captain Fantastic kurejea kwenye kiwango chake kile cha misimu mitatu nyuma.

 

bocco

bocco

Baada ya mchezo huo mashabiki mbalimbali waliandika jumbe zao kwenye ukurasa rasmi wa Klabu ya Simba SC, kumuomba msamaha John Bocco kutokana na wengi kati yao kuona kiwango chake kimeisha na hapaswi tena kuwa sehemu ya kikosi cha Simba.

Bocco alihojiwa baada ya Mechi kulingana na kiwango chake cha mechi hiyo, alijibu kuwa kila mechi wachezaji wanapambana kupata matokeo mazuri ya timu, hivyo yeye kama mchezaji anamshukuru Mungu na kila atakapokuwa anapata nafasi ya kucheza atahakikisha anatoa mchango kwa timu.

 

bocco

 

Simba SC Imepanda kileleni kwa kufikisha alama 27 na michezo 12, huku wapinzani wao Yanga wakiwa nafasi ya pili kwa alama 26 wakiwa na michezo miwili mkononi, ambapo mchezo wao unaofuata utakuwa dhidi ya Dodoma Jiji siku ya Jumanne Novemba 22.


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

machaguo spesho

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa