Mmemuona Messi? Bado Kuna Mjadala wa Nani Bora?

Lionel Messi alionyesha mchezo mwingine mzuri wakati Argentina ilipoifunga Croatia na kutinga fainali ya Kombe la Dunia, na nyota kadhaa wa soka wanaamini kuwa mjadala wa ‘GOAT’ ‘MBUZI’ sasa umekwisha.

 

MESSI

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alifunga bao na asisti mbili, akimtengenezea Julian Alvarez mara mbili, la pili likitokea baada ya kukimbia kwa kasi kutoka katikati ya mstari – huku Argentina ikishinda mabao 3-0 Jumanne usiku, na kulipa kisasi chao cha mwaka 2018 nchini Urusi walifungwa na Croatia bao 3-0 na Croatia kutinga hatua ya fainali ya Kombe la dunia.

Messi na Argentina walijikatia tiketi ya kucheza fainali ya Kombe la Dunia Jumapili, na Ufaransa au Morocco – ambao watacheza Jumatano usiku. Bashiri na kitochi au bila bando mechi hii, Bonyeza hapa kutazama ODDS kubwa na bomba kupitia machaguo spesho ya meridianbet ili kuingia mchezoni. Pia ukibashiri na kitochi kwa dau la TZS 1,000/= Unaweza kuibuka mshindi wa MBUZI WA KITOWEO CHA SIKUKUU, kila wiki Ijumaa.

 

MESSI

Sio tu kwamba Messi aliendesha mchezo huo, katika kufunga pia akawa mfungaji bora wa muda wote wa Kombe la Dunia la Argentina akiwa na mabao 11, akimpita Gabriel Batistuta aliyefunga 10.

Mchambuzi Gary Lineker, aliandika kwenye Twitter baada ya Messi kutoa pasi nzuri ya bao la pili la Alvarez, alisisitiza kuwa mjadala kuhusu kipaji bora zaidi ya muda wote wa soka sasa umekwisha. ‘Bado kuna mjadala? Kuomba mbuzi (GOAT),’ aliandika.

Jamie Carragher aliunga mkono maoni ya Lineker, na kuongeza: “Bora zaidi kuwahi kutokea!”

Naye Jeff Stelling, akielekeza ujumbe wake kwa shabiki na rafiki wa Cristiano Ronaldo Piers Morgan, aliongeza: “Kwa hiyo tuko wapi sasa kwenye mdahalo wa Ronaldo v Messi?”

Messi, katika kufunga dhidi ya Croatia, pia alilingana kwa mabao na nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha Kombe la Dunia nchini Qatar kwa mabao matano.

 

MESSI

 

Mshambuliaji huyo mkongwe pia amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga na kusaidia katika mechi nne tofauti kwenye Kombe la Dunia tangu toleo la 1966 la mashindano hayo.

Rekodi ya kimataifa ya Messi imekuwa ikishutumiwa kwa muda mrefu, huku wengi wakimchagua Muargentina mwenzake, Diego Maradona kama mchezaji wao bora zaidi, baada ya kuiwezesha nchi yake kushinda Kombe la Dunia mwaka 1986.

Fowadi huyo alikuwa na mchango mkubwa kwani Argentina ilishinda Copa America mwaka jana, hata hivyo, na kwa mara nyingine ametimiza jukumu muhimu nchini Qatar.

Bado kuna wale wanaomchagua gwiji wa Brazil Pele kama bora zaidi wa wakati wote, wakati Cristiano Ronaldo, bila shaka, pia yuko kwenye mjadala.

Mtu mmoja anayeshikilia nafasi ya Ronaldo kwenye mdahalo huo ni Piers Morgan, ambaye bado yuko juu kwenye orodha hiyo.

Aliandika kwenye Twitter: “Nafikiri Cristiano Ronaldo ndiye bora zaidi kuwahi kutokea, Maradona wa 2, Messi wa 3 (inawezekana wa 4, nyuma ya R9).”

Mfungaji bora wa muda wote wa EPL Alan Shearer aliongeza: “Ilikuwa ni furaha iliyoje kuwa uwanjani kutoa maoni kuhusu timu hii ya Argentina na mashabiki. Messi na Alvarez wanapendeza usiku wa leo.”

Acha ujumbe