Morocco Yatinga Hatua ya 16 Bora Baada ya Miaka 36

Timu ya Taifa ya Morocco kutoka Barani Afrika imetinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Dunia hapo jana baada ya kuichapa timu ya Taifa ya Canada kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa majira ya saa 12:00 jioni.

 

Morocco Yatinga Hatua ya 16 Bora Baada ya Miaka 36

Morocco ambayo ilikuwa katika Kundi F alishinda mechi zake mbili kwa kumtwanga Ubelgiji na Canada pamoja na kutoa sare moja dhidi ya Croatia na kufikisha pointi 7 kwenye msimamo kama kinara wa kundi hilo.

Katika kundi hilo anayefuata ni Croatia ambae naye pia ametinga hatua ya mtoano akiwa na pointi tano. Mara ya mwisho Morocco kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1986.

Morocco Yatinga Hatua ya 16 Bora Baada ya Miaka 36

Mechi ya mtoano watakipiga dhidi ya Hispania huku ushindi atakaopata utamfanya afike hatua ya robo fainali ya michuano hii, ambapo mechi hiyo inatarajiwa kupigwa siku ya Jumanne tarehe 6.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.