Kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Brazil Fred amefichua siri ambayo watu wengi walikua hawajui kuhusu kiungo mwenzake wa Kibrazil Carlos Casemiro.

Kiungo huyo amefunguka kua alijua kuhusu usajili wa kiungo Casemiro ndani ya klabu hiyo miezi kadhaa kabla ya klabu hizo mbili kukubaliana na kutangaza kusajiliwa kwa mchezaji huyo ndani ya United.

Ikumbukwe usajili wa kiungo Casemiro ulionekana kama ni usajili w kushtukiza na haukua kwenye mipango ya timu hiyo, na wengi wakidhani kama ni usajili ambao ulikua wa presha ndani ya timu hiyo lakini Fred anaeleza haikua hivo kwakua alijua muda mrefu hivo inaonesha ulikua usajili wa kimkakati.fredKiungo huyo anaeleza waliongea na Casemiro na kumuuliza ni namna gani ataishi katika klabu hiyo na Fred alimueleza kila kitu kuhusu timu hiyo kama alivyoeleza kiungo huyo.

Casemiro ambaye amejiunga na klabu hiyo dirisha la usajili lililopita la majira ya joto lakini mpaka sasa mchezaji huyo ameonesha mabadiliko makubwa kwenye safu ya kiungo ya klabu hiyo, Huku akifanikiwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba ndani ya klabu hiyo.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa