Klabu ya Manchester United inaripotiwa kuwa wanafikiria kumsajili nyota wa Barcelona Frenkie de Jong kama mbadala wa Paul Pogba.
Mashetani Wekundu mpaka sasa hawajafikia muafaka wa makubaliano ya mkataba mpya na nyota wao, Pogba. Staa huyu mwenye umri wa miaka 28 anafikia mwisho wa mkataba wake wa sasa msimu ujao wa joto.

Man United wapo mbioni kumpoteza staa wao kama mchezaji huru msimu ujao wa joto, wakati De Jong akihusiswa na kuondoka Barcelona katika siku za hivi karibuni akitajwa kuwa na thamani ya Euro milioni 75.
Vilabu vingi vya Ligi Kuu ya Uingereza vinamtupia macho nyota huyu, na huenda kukawa na mshike mshike kwenye dirisha la uhamisho la mwezi Januari.
Kwa mujibu wa Daily Mail, Man United wanajiandaa kupambana na Man City na Liverpool kuiwania saini ya Frenkie de Jong ambaye anaweza kuwa sokoni mwezi Januari.
Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.


