Klabu ya Manchester United bado iko ndotoni juu ya baadaye ya nyota wao na mlinda mlango, David de Gea endapo atakuwa tayari kuongeza kandarasi yake ili kuendelea kuitumikia klabu hiyo. Kandarasi ya raia huyo wa Hispania na mlinda mlango bora kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya soka inaisha msimu ujao na ifikapo Januari atakuwa huru kufikia makubaliano na klabu nyingine yoyote. Inaonekana lengo la nyota huyo ni kupima mwenendo wa kikosi hicho ili kujiaminisha anaposaini nao.
Barcelona wamethibitisha kwamba kwa sasa hawana nia yoyote ya kumuondoa Coutinho ndani ya kikosi chao na atakuwa kuru kusalia na kupambania namba na mataji ndani ya kikosi hicho. Hilo limekuja baada ya fununu za muda mrefu kwamba nyota huyo angeweza kutolewa kwa mkopo ili kupisha usajili wa Neymar. Na katika hilo inaonekana wameanza kujiweka mbali na usajili wa Mbrazil huyo kwa awamu nyingine.
Kiungo na raia wa Manchester United, Paul Pogba hana hakika kama atakuwa na maisha zaidi ndani ya kikosi cha timu hiyo kwa siku za mbeleni baada ya kuhusishwa sana na taarifa kutoka Madrid na Juventus wakiwa na nia ya kumsajili. Juventus wanatamani kufanya biashara tena na United juu ya nyota huyo. Japo nyota huyo pamoja na ripoti hizo amekiri kwamba haziwezi kumshushia morali wala kumfanya alete mgawanyiko kikosini hapo.
Inawezekana nyota wa Arsenal ambaye amedumu kwa misimu kadhaa kikosini hapo akaomba kuondoka kutokana na mahusiano yake na kocha wa sasa wa klabu hiyo kuwa siyo mazuri sana. Hadi sasa taarifa zinasema wawakilishi wake wamekwenda kukutana na klabu ya DC United ya Marekani ili kuona kama nyota huyo anaweza kujiunga na miamba hao wa soka ambako awali Rooney alikuwa akichezea.
Liverpool na Arsenal wanahusishwa na kutaka saini ya nyota wa Barcelona na raia wa Brazil, Rafinha kwa msimu ujao. Nyota huyo anatamani sana kwenda kupata klabu ambayo itampa namba ya kudumu mbali na ilivyo sasa akiwa ndani ya Barcelona. Mbali na klabu hizo mbili inaonekana kwamba Valencia wana nia ya kumsajili nyota huyo ili aweze kuhudumu kikosini kwao na wao kujiimarisha zaidi kiushindani. Hata Barcelona wanaonesha wapo huru kabisa kumuachia nyota huyo.
United wapo tayari kumuachia Darmian kuweza kujiunga na Inter Milan bila ada yoyote akiwa kama mchezaji huru ili awe huru kabisa kutimka kikosini hapo. Hiyo itakuwa biashara ya pili kufanya kati ya klabu hizo mbili baada ya ile ya Lukaku kufanikiwa. Kama ataondoka klabuni hapo kwa nafasi fulani atapata kuonekana zaidi uwanjani.


Povel tz
Gud news