Kivumbi cha ligi kuu ya Uingereza kati ya klabu mbili ambazo zina ushindani wa siku nyingi unategemewa kuonekana leo uwanjani ambapo itawakutanisha nyota wa klabu za Tottenham na Manchester City ambapo tambo za wawili hao zikishika nafasi hususan Pochettino ambaye anaonekana kutarajia makubwa ndani ya mechi hiyo.
Mechi hiyo ni sehemu ya mechi za mzunguko wa pili wa ligi kuu ambapo mechi nyingine kubwa iliyoshuhudiwa wiki lililopita ilikuwa ni kati ya United na Chelsea na hii itakuwa mechi nyingine kubwa ya pili inayowakutanisha wababe waliokuwa nafasi za juu za ligi katika msimu uliopita ambao watakuwa wakioneshana ukomavu kisoka.
City atakuwa mwenyeji wa mchezo huo ambapo atamkaribisha Spurs ambao kikosi chao kimeonekana kuwa tishio sana hivi karibuni na kuvunja historia ya kufanya vizuri sana kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya. Amefanya baadhi ya mabadiliko kwenye kikosi chake na atakuwa huru kufanya makubwa sana katika mchezo wake wa leo.
Wakati Pochettino akihojiwa juu ya mechi hiyo ya leo, ameweka utani kidogo kwa kusema anataka kukaa ulingoni kupigana na Pep ilikiwa ni utani wa wawili hao kuelekea mtanange unaosubiriwa na wapenzi wa soka duniani kuona maajabu ambayo wawili hao wanaweza kuyaweka uwanjani leo.
Manchester City kwa matokeo yake na uimara wa kikosi chake kwa misimu hii miwili iliyopita bado ana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kwa sababu kikosi chake hakijabadilika kabisa na kipo imara bado kuendeleza ubabe kwa awamu nyingine tena. Endapo klabu shindani zitashindwa kupambana mapema ndani ya ligi ili kujiwekea akiba ya alama na magoli lolote linaweza tokea hata ndani ya msimu huu.
Uimara wa kikosi cha Pochettino pia hautii wasiwasi kwa sababu bado ana wachezaji ambao aliwatumia kwa mafanikio makubwa sana hata ndani ya msimu uliopita na waliweza kuonesha ushindani mkubwa sana katika hilo; hivyo kwa upande mwingine kikosi hicho ni tishio bado ndani ya msimu huu.
Kubwa ni kusubiri dakika 90 za mchezo zitaendaje ndani ya mechi hiyo kulingana na historia ya vikosi hivyo viwili na historia za wawili hao wanapokutana uwanjani. Hilo ndilo kubwa lililosalia kwa mechi hiyo.


Mariam mtandama
Vizur
Issa
Hawa ni makocha wenye upinzani
Povel
Vita ni Vita mura