Eriksen anaonekana kusema ndiyo juu ya dili lake na Madrid, inasemekana Madrid tayari wamepiga hatua kumnasa nyota na kiungo mchezeshaji wa Tottenham mwenye uwezo wa aina yake na tayari hatua za mwanzo kabisa za dili hilo zimefikiwa huku kukiwa na kila dalili kwamba akapewa mkataba mnono utakaomuweka kikosini hapo kwa kipindi kirefu.
Taarifa zinaonesha kwamba Madrid wapo tayari kumwaga kiwango cha €80m ili kumnasa kiungo huyo jambo ambalo kwao kwa msimu huu sio kitu kinachoshindikana kutokana na utajiri wao na mapato ambayo kama klabu wanayo na wamefikia. Kwa hakika wanahitaji wachezaji wa aina yake ili kujiweka pazuri msimu ujao.
Inazidi kuonekana kwamba Madrid wapo tayari kumpa mkataba wa mwanzo kabisa wa miaka sita ndani ya klabu hiyo baada ya kuridhishwa na utendaji wake na hakuna dalili yoyote ya dili hilo kufeli kutokana na dau alilotengewa nyota huyo na aina ya klabu inayomuhitaji.
Nafasi yake ya kutua hapo inaweza kuziba kabisa matamanio ya ama Pogba au Juan Mata kujiunga na miamba hao ambao nao walikuwa wanahusishwa sana kutaka kujiunga na klabu hiyo. Eriksen akitua hapo kutakuwa na nafasi ndogo sana kwa wawili hao kuendelea kuwindwa.
Manchester United huenda wakafanya biashara nzuri kwa Lukaku, ni miongoni mwa nyota ambao wanatazamiwa kuachana na klabu hiyo baada ya kuwa na kiwango ambacho kwa hakika hakijadhihirisha aina ya malipo wanayopokea na uwezo wao halisi wakiwa uwanjani kwa kushindwa kabisa kuibeba klabu msimu huu.
Inter Milan wanaonekana kumuhitaji Lukaku kwa nafasi yao japo wanataka biashara ya mabadilishano ambapo atatua hapo kama mbadala huku ikifanyika biashara ile ya mabadilishano kati yake na Icardi ambaye amehitaji kupewa ruhusa ya kuachana na klabu hiyo kwa kipindi kirefu sasa.
Endapo United watafanikiwa kumnasa Icardi kwa biashara hiyo watakuwa wamelamba dume kwenye biashara hiyo. Maana ni mchezaji mwenye takwimu za juu sana ndani ya klabu hiyo pia ana heshima yake kubwa ndani ya taifa la Argentina pamoja na ripoti za hapa na pale juu yake.


Povel
Gud news
Njiku
Ipo poa kwa lukaku acha aende inter kwa kupigiwa sana makelele na mashabiki wa man u coz alivyotoka everton alikuwa fiti na kamwili kadogo hivyo alikuwa anajituma good je alivyokuja united alikuwa bonge na alikuwa sio mwepesi na alishindwa kupafomu vizuri akiwa na united
Gabriel
Habar njema sana 👍