Gabriel Jesus Aendeleza Rekodi Yake Epl.

Gabriel Jesus mshambuliaji wa klabu ya Arsenal anaendeleza rekodi yake katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kufunga katika mchezo wa leo dhidi ya Tottenham Hotspurs.

gabriel jesusMchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Manchester City ameiweka hai rekodi ya kufunga katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza na kutopoteza baada ya kufunga leo na kutopoteza katika mchezo huo hivo ni rasmi mchezaji huyo amecheza michezo 51 na kufunga magoli 63 akiwa katika vilabu viwili vya Manchester City na sasa Arsenal na kutopoteza mchezo wowote pale anapofunga.

Gabriel Jesus amekua na kiwango kizuri tangu atue kwa washika mitutu hao wa London baada ya kufunga magoli matano kunako ligi hiyo na kuiwezesha timu hiyo kuendelea kubaki kileleni mwa ligi hiyo.

gabriel jesusGabriel Jesus amekua miongoni mwa wachezaji muhimu katika klabu ya Arsenal baada ya kutoka katika klabu ya Manchester City na kuonesha mabadiliko makubwa katika kikosi hicho cha Mikel Arteta.

Acha ujumbe