Mshambulaiji wa klabu ya Arsenal Gabriel Jesus hatakaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha ya goti ambayo ameyapata hivi karibuni.
Mshambuliaji Gabriel Jesus amekua akisumbuliwa na majeraha ya goti mara kwa mara kitu ambacho kimekua kikimfanya kukosa michezo kadhaa ya klabu yake pamoja na timu yake ya taifa ya Brazil.Taarifa kutoka kwenye jopo la madaktari wa klabu hiyo zimeeeleza kua licha ya kupata jeraha la goti mchezaji huyo hatakaa nje ya uwanja kwa muda mrefu, Kwani jeraha alilolipata awamu hii sio kubwa sana.
Gabriel Jesus atakaa nje ya uwanja kwa muda mchache kwajili ya kuangalia maendeleo yake, Lakini hatakaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwakua hajapata majeraha makubwa kama ambayo yalimueka nje kwa kipindi kirefu miezi kadhaa nyuma.