Shirikisho la soka Italia wanatumaini wachezaji watapimwa virusi vya Corona mwanzoni wa Mei kabla ya msimu kuendelea.
Serie A imesimamishwa tangu Machi 9 kwasababu ya gonjwa la mlipuko Duniani.
Bado tarehe rasmi ya Ligi ya Italia kurejea haijajulikana, wakati imebakiwa mizunguko 12 hadi kumalizika kwake.
“Punde hali itakapokaa sawa, tutakamilisha ligi,” amesema Raisi wa Shirikisho Gabriele Gravina.

“Punde, tutakuwa na kikao, tutaanzisha mfumo ambao tutazungumza.
“Tutaanza, natumaini, mwanzoni mwa Mei ni kupima wachezaji na mzoezi yatafuata.
“Tutacheza wakati wa kiangazi? Hatuna kikomo lakini lengo letu ni kukamilisha Ligi.”
Italia ni moja ya nchi zilizo athirika sana na janga la Corona na wachezaji pamoja na vilabu vimeathirika sana.
Raisi wa Brescia, Massimo Cellino ambaye ipo mwishoni mwa msimamo wa ligi, amesema wapo tayari kutokucheza michezo iliyobaki, kama msimu utaendelea.


isha
Makala nzuri