Fowadi wa Chelsea, Olivier Giroud amebainisha kuwa anaweza kuwa anajiandaa na kufikiria uwezekano wa uhamisho wa kuelekea AC Milan katika dirisha la uhamisho la msimu huu wa joto.

Wiki iliyopita iliwekwa wazi kuwa mkataba wa Giroud umeongezwa kwa miezi 12 zaidi, ikionekana kama mpango wa kuelekea San Siro ndiyo umefika tamati kwa msimu ujao wa uhamisho.

olivier giroud

Hata hivyo, Giroud, ambaye amezungumza na waandishi wa habari juu ya hatma yake amesema kuwa Chelsea tayari walikuwa wameshapitisha suala la kuongeza mkataba wake mapema mwezi Julai, na wametangaza wiki iliyopita kwa sababu ya kuendana na sheria za EPL.

“Ni muhimu kukumbuka kuwa niliwapenda Marco van Basten na Andriy Shevchenko. Milan ni moja ya klabu kubwa Ulaya. Lakini, leo, sitazungumza juu ya hatma yangu na timu kwa sababu nimejikita kwenye mishe mishe za timu ya Ufaransa na Euro, ambayo inakuja haraka.”


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa