Gomes Aishukuru Simba Kwa imani

Kocha Mkuu Didier Gomes, amemshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji (Mo) na Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez kwa ushirikiano waliompa hadi kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, jana.

Kocha huyu wa Simba amesema uongozi wa klabu ukiongozwa na Mo na Barbara wamemuamini na kumpa ushirikiano mkubwa na ndiyo sababu iliyotufanya kutwaa ubingwa tukiwa na mechi mbili mkononi.

Gomes amesema kuwa mafanikio ya yeye kuwa kocha bora kunatokana na kiwango kizuri cha wachezaji bora. Didier pia amekimwagia sifa kikosi cha Simba kwa uimara wake huku akisema wamestahili kutwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.

Raia huyo wa Ufaransa amesema msimu huu tumekuwa bora na tumestahili kutwaa ubingwa kwa sababu ndiyo timu iliyofunga mabao mengi na kufungwa machache kuliko zote.

“Lazima tumshukuru Mwenyekiti wa Bodi na CEO Barbara kwa ushirikiano walionipa kwanza kuniamini naweza kuifundisha hii timu na kuipa mafanikio.

“Pia siwezi kuacha kuwataja wachezaji wangu kwenye ubingwa huu, huwezi kuwa kocha bora bila kuwa na wachezaji bora pia tulikuwa na kikosi imara. Tumestahili kuwa mabingwa msimu tulikuwa bora zaidi ya timu zote,” amesema Gomes.

Hadi sasa Simba imebakiza mechi tatu kukamilisha msimu wa Ligi 2020/21, michezo miwili ikiwa ya ligi na fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup itakayopigwa Julai 25, mkoani Kigoma.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.