Beki wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Morocco Achraf Hakimi anaamini klabu hiyo itafanya makubwa chini ya mastaa watatu wa klabu hiyo Messi, neymar, pamoja na Kylian Mbappe.

Utatu huo ndani ya klabu ya PSG mpaka sasa unaonekana kufanya vizuri haswa katika ligi ya mabingwa ulaya ambayo ndo imekua lengo kubwa la klabu hiyo. utatu huo mtakatifu mpaka sasa umeshahusika kwenye magoli 19 ya klabu hiyo kwenye ligi ya mabingwa ulaya tu.hakimiBeki huyo wa kulia alizungumza hayo jana wakati klabu hiyo ikipata ushindi wa magoli saba kwa mawili dhidi ya klabu ya Maccabi Haifa na mastaa hao kufunga magoli huku Mbappe akifunga magoli mawili na pasi mbili za mabao, Messi akifunga magoli mawili na pasi mbili za mabao huku Neymar akifunga goli moja.

Klabu ya PSG jana wamefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora rasmi jana baada ya kuifunga Maccabi Haifa. na kukaa kileleni mwa msimamo kundi hilo ambapo wanagongana alama na klabu ya Benfica lakini wao wakiongoza kwa tofauti ya magoli.hakimiHakimi alifanya mahojiano baada ya mchezo huo na kusifu ubora wa utatu huo na ndani ya klabu ya PSG na kuona ikifanya makubwa zaidi wakiwa na wachezaji hao kwenye ligi ya mabingwa ulaya.

Ukiachana na Hakimi lakini pia mwalimu Galtier amesifu ubora unaliooneshwa na timu yake siku ya jana lakini pia akimimina sifa kwa utatu huo mtakatifu ambao umekua tishio kwasasa barani ulaya.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa