Achraf Hakimi beki wa kulia wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Morocco amefunguka kua staa wa klabu huyo Lionel Messi sio tatizo klabuni hapo.

Messi ambaye alitoka klabu yake ya zamani ya Barcelona msimu uliomalizika na hakua na msimu sana katika viunga hivyo vya Parc de princes lakini msimu huu anaonekana kurejea katika ubora wake ambao watu wengi wameuzoea kwani mpaka sasa ana mabao matatu ya ligi kuu na pasi saba za mabao.

achraf hakimiHakimi anasema “ubora wa Messi ndo ulioiwezesha klabu hiyo kupata alama tatu muhimu dhidi ya Brest siku ya jana ambapo ni maono yake yalisababisha kupata goli baada ya kumtengenezea Nyemar nafasi ya bao pekee lililofanya tushinde mchezo”.

Hakimi aliendelea kwa kusema “Unapoomba mpira kwa Messi na asipokupa inapaswa kujua kuna mwingine yupo kwenye nafasi nzuri zaidi hilo sio tatizo na ndivyo Lionel alivyompa pasi Neymar leo”.

Messi anaonekana kuimarisha kiwango chake haswa kipindi hichi kombe la dunia likikaribia ili aweze kuisaidia timu yake ya taifa kufanya vizuri ambayo imekua kiu yake ya muda mrefu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa