Real Madrid wameendeleza wimbimla ushindi katika ligi kuu nchi Hispania maarufu kama La liga baada ya kuifunga klabu ya Real Mallorca goli nne kwa moja.

Baada ya ushindi huo Madrid wanakua wamechukua alama zote katika michezo yote waliyocheza kwenye La liga kwani wamecheza michezo mitano kushinda yote huku wakivuna alama 15 huku wakishika usukani wa ligi hiyo.

real madridReal Madrid ambao leo waliingia uwanjani bila ya mshambuliaji wao nyota Karim Benzema anaesumbuliwa na majeraha ya nyama za paja walitoka nyuma na kuweza kupata ushindi huo mnono.

Mallorca walifanikiwa kupata bao kuongoza kwa Murigi dakika ya 35 ya mchezo kabla ya Fede Valverde kusawazisha na matokeo kwenda moja kwa moja mpaka kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Ni Vinicius alieiweka Madrid mbele kwa kufunga bao la pili dakika ya 72 kabla ya Rodrygo kufunga goli la tatu na beki Antony Rudiger kuhitimisha karamu ya mabao kwa kufunga goli la nne la mchezo dakika za nyongeza.

Mabingwa hao watetezi wanabaki kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baaada ya kushinda michezo yote walijitupa uwanjani msimu huu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa