Harry Kane Aikamia Arsenal

Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane ameonekana kuikamia Arsenal kuelekea mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya utakaopigwa kesho katika dimba la Allianz Arena.

Harry Kane amesema anatarajia kuonesha ubora mkubwa katika mchezo wa kesho kwani unaweza kuwapa fursa ya kucheza fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu huu baada ya kulikosa taji la Bundesliga.harry kane“Bundeliga imekua uzoefu mzuri kwangu,ninapenda kucheza Ujerumani kama tutafanya vizuri katika mchezo wa kesho itabaki michezo michache kucheza fainali ya ligi ya mabingwa ulaya Wembley, Nataka kuonesha kiwango bora kabisa katika mchezo huo”

Kutokana na kauli hiyo ambayo ameitoa mshambuliaji huyo kinara wa mabao wa Bundesliga ni wazi ameng’atia meno klabu ya Arsenal katika mchezo wa kesho, Lakini pia inaonesha akili yote ya klabu hiyo imehamia katika ligi ya mabingwa barani ulaya kwani hakuna kombe lingine ambalo wanaweza kutwaa msimu huu.harry kaneMshambuliaji Harry Kane amekua na takwimu nzuri sana pindi anapokutana na klabu ya Arsenal, Kwani mpaka sasa ndio mshambuliaji anayeongoza kufunga katika North London Derby ambayo inahusisha vilabu  vya Arsenal na Tottenham akiwa na 14 hivo inaonesha kua anaweza kufanya makubwa katika mchezo wa kesho.

Acha ujumbe