CEO Bayern Leverkusen Anamuona Alonso Akiinoa Madrid

CEO wa klabu ya Bayern Leverkusen Carro ameweka wazi kua anamuona kocha wa klabu hiyo Xabi Alonso akija kuifundisha klabu ya Real Madrid siku za mbeleni ila hajajua ni lini.

CEO Carro anaamini kituo kinachofuata kwa Xabi Alonso baada ya kuondoka ndani ya klabu ya Bayern Leverkusen ni klabu ya Real Madrid ambayo kocha huyo amewahi kuitumikia kwa mafanikio makubwa kama mchezaji.bayern leverkusen“Sina shaka siku moja Alonso atajiunga na Real Madrid kama kocha wa timu shaka kwenye hilo ni sifuri kabisa, Shaka iliyopo ni lini atajiunga lakini itakua hivo niamini nina uhakika” Ameyazungumza hayo CEO Carro.

Kocha Xabi Alonso siku kadhaa amekua akihusishwa na vilabu vya Liverpool na klabu ya Fc Bayern Munich ambavyo vyote amewahi kuvitumikia kama mchezaji kabla ya kutangaza hataondoka ndani ya Leverkusen msimu ujao, Huku akiahidi kuendelea kuwepo ndani ya klabu hiyo mabingwa wapya wa Ujerumani.bayern leverkusenTaarifa za ndani zinaeleza kocha Xabi Alonso ameshakubaliana mkataba wa awali na klabu ya Real Madrid punde tu mkataba wa kocha Ancelotti ukimalizika ajiunge na klabu hiyo, Huku ikiwa ndio sababu kubwa ya kocha huyo kukubali kusalia ndani ya klabu ya Bayern Leverkusen kwa msimu mmoja zaidi.

Acha ujumbe