Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amempongeza mchezaji wake Jadon Sancho ambaye anakipiga kwenye klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa mkopo.
Kocha Ten Hag amempongeza Sancho kutokana na ubora ambao ameuonesha ndani ya Borussia Dortmund na kuisaidia klabu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya.Kocha huyo akifanya mahojiano na wanahabari leo aliulizwa kama kiwango cha Sancho kimemfanya kubadilisha mawazo yake na majibu yake yalikua hivi”Hapana tunajua Sancho ni mchezaji mzuri sana hivo sio jambo la kushangaza kwetu, Amekua na mchango mzuri sana kwa Dortmund amekua na kiwango bora kwakweli”
Ikumbukwe chanzo cha winga Jadon Sancho kuondoka ndani ya Man United ni kupishana na kocha wake Ten Hag baada ya kutokupata nafasi ya kuanza katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Arsenal jambo ambalo lilipelekea kukosekana kwa maelewano baina ya wawili hao.Kauli ya kocha huyo raia wa kimataifa wa Uholanzi juu ya Sancho inatoa taswira ya kua huenda wawili hao wamemaliza tofauti zao hivo mwisho wa msimu winga huyo anaweza kurejea ndani ya kikosi cha Man United na kuanza kupata nafasi ya kucheza.